Joshua 13:15-20

15Haya ndiyo maeneo ambayo Musa alikuwa amewapa kabila la Reubeni ukoo kwa ukoo:

16 aEneo la Aroeri lililo ukingoni mwa Bonde la Arnoni, na kuanzia mji ulio katikati ya bonde, pia uwanda wote wa juu kupita Medeba 17 bhadi Heshboni na miji yake yote kwenye uwanda wa juu, ikijumlishwa miji ya Diboni, Bamoth-Baali, Beth-Baal-Meoni, 18 cYahasa, Kedemothi, Mefaathi, 19 dKiriathaimu, Sibma, Sereth-Shahari juu ya kilima kilicho katika bonde, 20 eBeth-Peori, materemko ya Pisga na Beth-Yeshimothi:
Copyright information for SwhKC